DKT JUMA MALIK AKIL AFANYA ZIARA KATIKA OFISI ZA ZIAAT
POSTED ON: 04-02-2026
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Juma Malik Akil leo tarehe 04 Februari. 2026 amefanya ziara katika Ofisi za ZIAAT na kuzungumza na Wajumbe wa Bodi na Watendaji wa taasisi hiyo
Mhe. Waziri ameeleza kuwa ZIAAT ni taasisi ya kitaaluma ambayo mpka sasa ina miaka miwili tu lakini imefanya mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kusajili jumla ya Wanachama 810 pamoja na kuanzisha Mitihani ya Taaluma ya Kodi
Aidha, Dkt Juma ameendelea kueleza kuwa ZIAAT inapaswa kujitegemea ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwake
Pamoja na mambo mengine Mhe. Waziri ameitaka ZIAAT kusimamia taaluma za kodi na Ukaguzi kwa umakini ili taaluma hizo ziendelee kufanya kazi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuwapatia mafunzo wanachama wake