MAFUNZO YA WAJUMBE WA BODI NA KAMATI ZA UKAGUZI
POSTED ON: 17-12-2025
Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi Zanzibar (ZIAAT) na Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar (TRO) wameendesha mafunzo ya siku mbili kwa Wajumbe wa Bodi na Kamati za Ukaguzi za Taasisi mbalimbali Zanzibar
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wajumbe wa bodi na wajumbe wa kamati za ukaguzi ili waweze kupitia nyaraka na ripoti za ukaguzi kwa ufanisi na uwelewa mzuri kwenye taasisi zao
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameishauri ZIAAT kuendelea kuwapatia mafunzo kama hayo mara kwa mara ili kuwajengea uwezo na kufanya kazi zao kwa ufanisi