ZIAAT YAKUTNA NA UONGOZI WA WIZARA YA ELIMU ZANZIBAR

POSTED ON: 06-11-2025

Uongozi wa Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi Zanzibar (ZIAAT) leo tarehe 06 Novemba, 2025 umekutana na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Lengo la ZIAAT kukutana na Wizara ya Elimu ni kujitambulisha pamoja na mambo mengine ambapo Mkurugenzi Idara ya Rasilimali watu, Utawala na Mipango CPA Rukia Hmad Abdulla ameeleza kuwa ZIAAT ni taasisi inayosimamia taaluma ya Uhasibu na Wahasibu, hivyo kuna haja kwa Wizara ya Elimu kushirikiana na ZIAAT katika maeneo tofauti hasa ya taaluma, miradi ya elimu, Tafiti mbali mbali pamoja na masuala ya kuboresha mitaala ya elimu Aidha, Naibu Katibu MKuu wizara ya Elimu Ndg. Khalid Masoud ameeleza kuwa kuna haja kubwa ZIAAT na Wizara ya Elimu kushirikiana kwani kuna walimu wanafundisha masomo ya uhasibu na wengine wanafanya kazi za uhasibu lakini hawana taaluma ya uhasibu, kushirkiana katika tafiti za elimu pamoja na kuwapatia mafunzo wahasibu na wakaguzi wote wa wizara ya elimu