ZIAAT YAKUTANA NA ZNCC

POSTED ON: 05-11-2025

Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa Kodi Zanzibar (ZIAAT) leo tarehe 04 Novemba, 2025 imekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Jumuiya ya kitaifa ya wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC) Mkurugenzi Rasilimali watu, Utawala na Mipango CPA Rukia Hamad Abdulla ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kuitambulisha ZIAAT kwa ZNCC pamoja na kufanya majadiliano ya namna bora ya kushirikiana na ZIAAT katika kazi mbali mbali kwani ZIAAT ina wanachama katika taasisi binafsi na serikalini Nae, Mkurugenzi Mtendaji wa ZNCC Ndg. Hamad Hamad ameeleza kuwa kuna haja kubwa ZIAAT kushirkiana na ZNCC kwani kuna wafanyabiashara wengi wanahitaji kupatiwa elimu ya Uhasibu na biashara pamoja na ushauri wa masuala ya kodi Aidha, Ndg. Hamad ameendelea kueleza kuwa katika Mkutano Mkuu wa ZNCC itatoa fursa maalum kwa ZIAAT kwa ajili ya kuwasilisha mada ili iweze kutambulika zaidi, Bw. Hamad ameeleza hayo leo mapema tarehe 04 Novemba, 2025 katika Ukumbi wa ZNCC Kinazini, Mjini Zanzibar