ZIAAT YAKUTANA NA KITENGO CHA KUDHIBITI FEDHA HARAMU TANZANIA (FIU)

POSTED ON: 26-09-2025

Mkurugenzi Mtendaji wa ZIAAT CPA Ame B. Shadhil leo tarehe 26 Septemba, 2025 amekutana na Naibu Kamishna wa Kitengo cha Kudhibi Fedha Haramu Tanzania Ndg. Seif Omar Hajji (katikati) CPA Ame B. Shadhil amemueleza Naibu Kamishna kuwa ZIAAT ni taasisi inayosimamia taaluma ya Uhasibu na Wahasibu, hivyo kuna haja kubwa kati ya ZIAAT na FIU kushirikiana katika kazi zao. Nae, Naibu Kamishna ameeleza kuwa ili kushirikiana vizuri kati ya ZIAAT na FIU kuna haja ya kufunga Mkataba wa mashirikiano (MoU) ili kufanikisha muonekano mpya wa mashirikiano