ZIAAT YATOA UWELEWA WA TAALUMA YA KODI
POSTED ON: 25-09-2025
Mjumbe wa Kamati ya Mitihani ya ZIAAT Ndg. Bakar SH. Bakar akitoa ufafanuzi wa taaluma za kodi zilizoanzishwa na ZIAAT tarehe 17 Septemba, 2025 katika ukumbi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ofisi ya Zanzibar
Ndg. Bakar ameeleza kuwa kwa sasa ZIAAT imeanza kufundisha taaluma za kodi ngazi ya awali na ngazi ya juu (Certified tax technician & Certified tax professional), hivyo ni fursa muhimu kwa maafisa kodi, wahasibu pamoja na wakaguzi na wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na kidatu cha sita