WANACHAMA WA ZIAAT WAENDELEA KUPATIWA MAFUNZO YA MFUMO WA PSMIS
POSTED ON: 08-09-2025
Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri Elekezi wa kodi Zanzibar leo tarehe 01 juni, 2025 imeendelea na kutoa mafunzo ya utumiaji wa mfumo wa usajili wa wanachama huduma kwa wateja (Professional Services Management Information System)Mafunzo hayo ya siku mbili yalianza tarehe 31 juni, 2025 hadi tarehe 01 juni, 2025 katika Ukumbi wa Tume ya Mipango Zanzibar.Baadhi ya wanachama wa ZIAAT waliopatiwa mafunzo wameeleza kuwa mfumo huu ni mfumo rafiki na utawawezesha kutumia muda mfupi kujisajili kupitia mfumo huu, kuomba namba ya malipo, kuliupia ada ya usajili na ya ada ya mwaka pamoja na kupata cheti kupitia kwenye mfumo